Prayers & Worships

Kitabu cha sala

avatar

Sala ya Kuombea Taifa letu

Mungu mwenye enzi, uyatawalaye mataifa yote na kuyaamrisha kama utakavyo. tunakuomba umbariki na kumwongoza rais wetu, na viongozi wote wa taifa letu, ili siku zote watumie mamlaka ulivyowakabidhi kwa ajili ya kuleta amani duniani, na kwa faida, heshima na ustawi wa taifa letu, na kwa wema wa kanisa lako takatifu; twaomba haya kwa kristo Bwana wetu. Amen
avatar

SALA YA KUOMBA NEEMA

Mungu Mwenye enzi, Umekua mlinzi usiku kucha, utulinde mchana kutwa; tuwe nuruni, na mashahidi wa njia zako, tuutafute ufalme wako kwanza na tukuone katika kila mmoja wetu; tuongoze katika njia za mwanao, na kutuelekeza kwenye mapito ya siku ya Bwana. kwa Kristo Bwana wetu. Amin.
avatar

SALA YA KUOMBA AMANI

Mungu mwenye enzi, na uishiye milele, Baba na Mfalme wa amani, Katika utulivu na kujirudi twaokolewa, katika ukimya na tumaini twapata nguvu. Utupe Baraka za kutaka kuwa na maridhiano na amani, na furaha ya kutafuta haki. Tuondolee mioyoni mwetu dhiki na taabu zote, uyafanye maisha yetu yashuhudie uzuri wa amani; tunakuomba kwa jina la Yesu Kristo Bwana wetu. Amin.
avatar

SALA YA KRISOSTOMO MTAKATIFU

Mungu Mwenye enzi, uliyetupa neema wakati huu tushirikiane kukuletea maombi yetu kwa moyo mmoja; umeahidi ya kwamba watu wawili au watatu wakusanyikapo katika jina lako, utawapa mahitaji yao. Uyatimize sasa ee Bwana, maombi ya watumishi wako kwa jinsi itakavyotufaa, ukitujalia tuijue kweli yako katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika zamani zijazo kwa Kristo Bwana wetu. Amin.

Add your prayer

About

We strive to empower Gods people to transform society through christ for holistics life, guided by our core values of servant leadership, integrity, commitment, teamwork, inclusivity, time management, embracing technology, innovation and creativity.